Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo video. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo video. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 10 Juni 2016

Chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya yatoa kauli ya kumuunga mkono naibu spika



Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya iliyokutana tarehe 04.06.2016, ilitoka na maazimia yafuatayo.
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, Inampongeza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson Mwansasu, kwa jinsi anavyolisimamia na kuliongoza Bunge kwa kufuata na kusimamia misingi ya sheria, taratibu na kanuni za Bunge.

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha Wabunge wa vyama vya upinzani kuonyesha utovu wa nidhamu kwa Bunge kwa kutoheshimu kiti cha Spika.


Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha wabunge wa vyama vya upinzani kutoka nje wakati wa vikao vya Bunge na kwenda kupiga soga nje, huku wakijua kuwa wametumwa na wananchi kwenda Bungeni kuwawakilisha.

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha wabunge wa upinzani kuendesha siasa Bungeni, badala ya kufanya kazi ya kutunga sheria na kuisimamia Serikali.


Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani matamko ya wabunge wa vyama vya upinzani, ya kuzunguka nchi nzima kwenda kufanya siasa za kuwahadaa wananchi kuwa wameonewa, wakati wao ndio hawataki kufuata kanuni na taratibu za Bunge.
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, Inaunga mkono hatua ya Uongozi wa Bunge kutowalipa posho wabunge wote watakaokuwa wanatoka Bungeni bila ya kufuata utaratibu.

WATUMISHI HEWA 170 WAPATIKANA MBEYA


Serikali Mkoa wa Mbeya imebaini watumishi hewa 170 kutokana na uhakiki ulifanywana timu ya vyombo vya dola iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa mbeya tarehe 20 April mwaka huu na idadi ya watumishi hewa imesababisha hasara ya she 773,882,066

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya alipokutana na waandishi wa habari kutangaza matokeo ya timu aliyounda kuhakiki watumishi hewa

Pamoja na hasara hiyo watumishi hewa 58 kati ya 170 wamekopa mikopo katika benki jumla ya shilingi 481,574,351

Serikali pamoja na kufanya uhakiki iliwataka watuhumiwa kurejesha fedha zote katika akaunti na sh 65,058,542

Mkuu wa mkoa amewaagiza wakurugenzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuwasaka popote walipo watumishi hewa na kuwachukulia hatua za kisheria

Aidha amewaagiza wakurugenzi, maafisa utumishi na maafisa wa mfumo kuwajibika kwa kuendelea kulipa watumishi hewa

Kuanzia sasa kila afisa utumishi atawajibika kuwaondoa watumishi watoro pale wanapobainika na amewataka wakurugenzi kuwa na mipango endelevu ya kudhibiti watumishi hewa.