Ijumaa, 10 Juni 2016

Chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya yatoa kauli ya kumuunga mkono naibu spika



Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya iliyokutana tarehe 04.06.2016, ilitoka na maazimia yafuatayo.
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, Inampongeza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson Mwansasu, kwa jinsi anavyolisimamia na kuliongoza Bunge kwa kufuata na kusimamia misingi ya sheria, taratibu na kanuni za Bunge.

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha Wabunge wa vyama vya upinzani kuonyesha utovu wa nidhamu kwa Bunge kwa kutoheshimu kiti cha Spika.


Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha wabunge wa vyama vya upinzani kutoka nje wakati wa vikao vya Bunge na kwenda kupiga soga nje, huku wakijua kuwa wametumwa na wananchi kwenda Bungeni kuwawakilisha.

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani kitendo cha wabunge wa upinzani kuendesha siasa Bungeni, badala ya kufanya kazi ya kutunga sheria na kuisimamia Serikali.


Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, inalaani matamko ya wabunge wa vyama vya upinzani, ya kuzunguka nchi nzima kwenda kufanya siasa za kuwahadaa wananchi kuwa wameonewa, wakati wao ndio hawataki kufuata kanuni na taratibu za Bunge.
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya, Inaunga mkono hatua ya Uongozi wa Bunge kutowalipa posho wabunge wote watakaokuwa wanatoka Bungeni bila ya kufuata utaratibu.