Jumamosi, 1 Agosti 2015

MGOMBEA URAIS KUPITIA UKAWA NA MWANACHAMA WA CHADEMA EDWARD LOWASSA LEO ANATARAJIWA KURUDISHA FOMU YA URAIS

 Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa leo Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.
Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara itakayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.
Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.
Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.