Mgombea Udiwani Kata ya Maendeleo Penieli Mwaisango leo alikuwa akiwaomba kura wakazi wa kata ya maendeleo kumpa kura za kutosha ifikapo tarehe moja mwezi ujao .Moja ya ahadi alizotoa ni kufuatilia Mapato yanayoingizwa na ukumbi wa mikutano wa Benjamini Mkapa na kisha kujua kata ya maendeleo inanufaikaje na pato linaloingia kwenye ukumbi huo.Pia alisema akipata nafasi yeye atafanya kazi kwa vitendo na si mazungumzo ,pia alizungumzia kuhusu michezo kwa vijana kuweza kulekebisha uwanja wa michezo kwa vijana na kurudisha hamasa ya michezo katika eneo la Kiwanja Ngoma lililopo katika kata ya maendeleo iliyopo Sokomatola Mbeya
Mgombea Udiwani kata ya Maendeleo Mtawa Kapalata alisema endapo atapata nafasi ya kuteuliwa na chama chake ni kuludisha eneo laShule ya Loleza kurudi kwenye kata ya maendeleo kama ilivyokuwa Zamani ,pia alizungumzia Makazi ya sokomatola kuakikisha Hati waliyopewa ni ya Mwaka Mmoja hivyo alikuwa anaomba nafasi ya kuteuliwa na chama chake ili aweze kufuatilia swala ilo kwa umakini na kupata Ofa ya muda mrefu.Mtawa alikwenda mbali na kusema wananchi wampe nafasi ya kugombea kwa mara nyingine kwani toka mwaka 2000 anagombea nafasi hiyo,.
Mgombea Udiwani anayetetea nafasi yake kwa kipindi kingine Modest shiyo alionekana kupata wakati mgumu pale alipoulizwa kuhusu endapo hatakosa nafasi je atashilikiana na wenzake alisema kama kutatokea tofauti ya matokeo awezi kuungana na mgombea atakayepitishwa ,lakini pia baadae alikuja kuomba radhi na kusema alipitiwa na kufuta kauli hiyo,hata hivyo shiyo alionekana kupaniki mara kwa mara kutokana na kuulizwa maswali na wanachama wa CCM ilifika kipindi alihoji huyu ni mkazi wa wapi ikabidi mwenyekiti wa kata kumweleza amuache mwanachama aendelee kuuliza swali.Pamoja na hayo shiyo alikutana na maswali magumu moja ya swali aliloulizwa ni kitu gani alichowafanyia na kitakachowafanya wakazi wake wamkumbuke ,alisema amewaletea Magorofa ya chama cha walimu pia amejenga barabara ya stendi ya daladala ya Sokomatola hadi kwenye kituo cha afya cha (Kiwanja Mpaka) kupitiaSerikali ya chama chake pamoja na Chuo cha Utumishi.