Jumamosi, 4 Aprili 2015

KAMPUNI YA ASAKYS YAANZA KWA KASI KUFANYA KAZI YAKE KATIKA KATA YA SISIMBA


Kampuni ya ASAKYS INVESTMENT imeanza kazi yake ya kuzoa taka  katika kata ya SISIMBA siku ya leo Akitoa wito mbele ya ya waandishi wa habari Meneja oparesheni Ayasi njarambaa  amewaomba wanachi kuacha kutupa taka kwenye maguba kama ilivyozoeleka hapo nyuma na kufuata utaratibu mpya  wa ukusanyaji taka ambapo kuna vifaa maalum vitawekwa katika mitaa ambayo kampuni yake imepata tenda ya kuzoa taka ikiwa ni kata ya FOREST na SISIMBA amewaomba wakazi wa kata hizo mbili kufuata anbazo zimetolewa na kampuni yake ,pia ametoa ratiba ya kuja kuchukuliwa taka katika kata ya SISIMBA  kama ifutavyo:jumatatu ni mtaa wa tanesco na soko kuu,jumanne jakaranda A na B jumatano ni uzunguni A na B na siku ya ijumaa ni siku maalum ya Stendi kuu.

Naye diwani wa kata ya sisimba Mh.kajigiri amewaomba wananchi wa kata yake kutoa ushirikiano na kampuni ya ASAKYS INVESTMENT ili iwe rahisi kufanya kazi na kufanya kata yake iwe kata ya kuigwa kama ilivyo katika mji wa moshi