kama unavyojionea haya ni baadhi ya maduka mkoani mbeya ambayo yamekuwa ni kero kwa wakazi wake.mmoja ya vitu ambavyo vimekuwa ni kero mkoani mbeya hasa maeneo ya mwanjelwa ni upigaji wa muziki pamoja na matangazo ambayo yamekuwa kama matangazo ya barabarani mmoja ya wateja ambaye aliongea na harubu tz asubuhi ya leo amesema wanaiomba halmshauri ya jiji la mbeya kuangalia taratibu ya kudhibiti makelele ya wafanyabiashara wa simu mkoani humo kwa vile tayari imeshakuwa dili kwa wafanyabiashara hao kufungulia sauti kubwa na kushindwa kusikilizana duka moja na jingine harubutz leo itakutana na mkurugenzi wa jiji la mbeya na kujua kama sheria ya kupiga matangazo na mziki vimeruhusiwa hadharani bila kibali chochote.