Jumatano, 17 Juni 2015

mh waziri mkuu mizengo pinda leo mkoani mbeya amepata wadhamini 2644

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ambaye pia ametangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amepata wadhamini 2644
Akitoa nasaha zake kwa wakazi hao leo (Jumatano, Juni 17, 2015), Waziri Mkuu aliwashukuru wote waliomdhamini huku akiwaomba waendelee kumuombea safari zote zilizo mbele yake na zoezi zima liende vizuri kwani suala la urais siyo lelemama bali ni la kumtanguliza Mungu.

Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Suala la urais si la kufa na kupona bali ni la kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwanza. Kila mgombea anapaswa amuombe Mungu kwamba kama itampendezea na kumuona anafaa ndipo amchague yeye (mtangaza nia).”

“Ndiyo maana mara zote huwa nawaambia wenzangu kwamba hakuna haja ya kutukanana wala kupakana matope. Huwa nawaambia tusikwaruzane wala tusitukanane kwa sababu hakuna ajuaye Mwenyezi Mungu amemuandaa nani miongoni mwetu,” alisema.

Aliwataka wananchi na viongozi wa wilaya hiyo watoe ushirikiano kwa wagombea wengine watakaofika mkoani humo kuomba wadhamini.